Pages

TUNAJIUSISHA NA HABARI ZA AINA ZOTE NDANI NA NJE YA BONGO VILEVILE TUNAKODISHA VYOMBO VYA MUZIKI NA P.A MAENEO YOTE YA JIJI LA MWANZA NA NJE YA JIJI LA MWANZA KARIBUNI SANA

MMMH...MAKUBWA NA MAZITO HAYA....HILI NDILO BALAA LA SIKUKUU YA WAPENDANAO "VALENTINE DAY" KWA WADOSI...SOMA ZAIDI HAPA


Wahindu wenye msimamo mkali wameonya kuwashambulia wahindi watakaosherehekea siku ya wapendanao "Valentine Day " kwakuwa sherehe hizo ni kinyume na utamaduni wa kihindi.

Wanamgambo wanaojiita Sri Ram Sena ambao wanadai wanalinda utamaduni wa wahindi walisema kwamba siku ya Valentine si kwaajili ya raia wa India.

Vitisho hivyo vimekuja siku chache baada ya kundi hilo kuvamia baa moja katika mji wa Mangalore na kumtoa nje ya baa hiyo mwanamke mmoja kabla ya kumpiga kwa madai kwamba ametoka nje ya maadili.

Shambulio hilo lilileta wasiwasi kwamba wanaharakati wa "Hindu Taliban" wameanza kuongezeka nchini India.

Gangadhar Kulkarni, mwanaharakati wa kundi hilo alisema kwamba "Kama watu watasherehekea siku ya Valentine pamoja na sisi kuwaonya, bila shaka tutawashambulia".

"Siku ya Valentine siyo utamaduni wa wahindi kwahiyo hatutaruhusu sherehe hizo zifanyike kwa njia yeyote ile" alidokeza Pramod Mutalik mwanzilishi wa kundi hilo.

Makundi kadhaa ya wahindu yamekuwa yakiwashambulia wale wote wanaoonekana kufuata utamaduni wa kimagharibi.

0 comments:

Chapisha Maoni