Pages

TUNAJIUSISHA NA HABARI ZA AINA ZOTE NDANI NA NJE YA BONGO VILEVILE TUNAKODISHA VYOMBO VYA MUZIKI NA P.A MAENEO YOTE YA JIJI LA MWANZA NA NJE YA JIJI LA MWANZA KARIBUNI SANA

JAMAN POMBE SIO CHAI' LULU ASISITIZA ANADAI ANAIOGOPA ZAIDI YA UKOMA...


MSANII wa filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amesema kuwa sasa hivi anaiogopa na kuiheshimu sana pombe akiamini kwamba ndiyo chanzo cha maisha kuharibika.
Kwa mujibu wa tovuti ya GPL hivi , Lulu alisema tangu ametoka gerezani ameamua kujiweka pembeni na kilevi hicho na kwamba bora aitwe mshamba.
“Kiukweli nikiiona pombe kuna wakati naipa shikamoo kwani ndiyo kichocheo cha kila baya hapa duniani, watakaoniona mshamba kwa kubadilika kwangu wanione hivyohivyo,” alisema Lulu.
Msanii huyo kipindi cha nyumba alikuwa hakamatiki kwa kilevi na kuna wakati aliwahi kuzimika alipofakamia pombe za ofa alipokuwa ndani ya Ukumbi wa Maisha Club, jijini Dar.

0 comments:

Chapisha Maoni