Pages

TUNAJIUSISHA NA HABARI ZA AINA ZOTE NDANI NA NJE YA BONGO VILEVILE TUNAKODISHA VYOMBO VYA MUZIKI NA P.A MAENEO YOTE YA JIJI LA MWANZA NA NJE YA JIJI LA MWANZA KARIBUNI SANA

Mwandishi wa gazeti la MWANANCHI akatwa katwa mapanga mkoani SINGIDA

Mwandishi wa habari wa gazeti la The Citizen na mwananchi mkoani Singida, Awila Silla amenusurika kuuawa na mtu anayedhaniwa kuwa Jambazi baada ya kukatwa katwa  mapanga kichwani na kusababisha kuzirai. Tukio hilo limetokea juzi saa mbili usiku jirani na mahakama ya mwanzo ya Utemini mjini Singida. 

Awila ambaye amelazwa wodi 2   katika hospitali ya mkoa amedai kuwa  baada ya kukutana na kijana huyo aliamuriwa kutoa fedha na baada ya kudai hana, jibu hilo lilisababisha kijana huyo kuanza kumkata Mapanga na alipoangauka na kuzirai alinyang’anywa  simu yake ya  kiganjani .

Hata hivyo Awila amedai kuwa bado hajatoa taarifa ya tukio hilo polisi

0 comments:

Chapisha Maoni