Mtu
mmoja anaesadikiwa kuwa ni jambazi ambaye hakufahamika jina
anayekadiliwa kuwa na umri wa miaka 25 ameuwawa kwa kupigwa mawe kisha
kuchomwa moto na mwingine kunusurika kuuwawa. Tukio hilo limetokea jana
alfajiri katika kijiji cha Shibula kata ya Bugongwa wilayani Ilemela
Mkoani Mwanza kufuatia tukio la wizi lilotokea usiku wa kuamkia jana
katika mtaa wa Nyamwilolelwa ambapo pikipiki moja na paneli ya solar
ziliibiwa. Katibu wa Sungusungu katika kijiji cha Shibula John Mashalia
amesema kuwa kufuatia tukio hilo waliamua kuweka ulinzi shirikishi
kuzunguka vijiji vyote na ndipo walipokutana na kijana huyo aliyeuwawa
akiwa na kijana mwingine aliyefahamika kwa jina la Edward Aloyce ambao
walidai wanatafuta pikipiki iliyopotea. Mashalia ameongeza kuwa kata ya
Bugongwa imekuwa na matukio ya ujambazi mara kwa mara ikiwa ni pamoja na
vitendo vya ubakaji kwa watoto na wanawake. Kwa upande wake mkaguzi
msaidizi wa jeshi la polisi Joyce Kotecha amewataka wananchi wa kata
hiyo kuacha kujichulia sheria mkononi na kwamba wawasiliane na uongozi
wa kata yanapotokea matatizo ya namna hiyo.
Kijana aliyeuawa kwa kuchomwa moto
Vijana wa sungusungu wakiwa katika mlango wa duka ambapo kijana mwingine aliyenusurika alifungiwa kungoja polisi waje
Hii ni pikipiki ambayo vijana hao walienda nayo eneo la tukio
Polisi wakipanga jinsi ya kumtoa mtuhumiwa huyo
Ambulance ikiandaliwa kupakia maiti ya kijana huyo....
Polisi wakikagua makoti ambayo kijana aliyenusurika alikuwa ameyavaa
Kijana aliyenusurika aitwaye Mangi akitolewa ndani ya duka kwa ulinzi mkali na kupakiwa kwenye gari...
Kijana Mangi akiwa ndani ya gari, pembeni yake ni maiti ya mwenzake....









0 comments:
Chapisha Maoni