Kuishi nyumba ya kupanga:
Tangu alipopata mafanikio ya kimuziki (2010-2014) Diamond amekuwa akiishi numba ya kupanga baadaya kuihama
nyumba ya bibi yake iliyoko Tandale (katikati ya kituo cha Shule na
Tanesco.) baaba ya hapo alihamia mitaa ya Sinza Madukani upande wa kulia kama unatoka Shekilango kuelekea Mwenge.
Nyota ilivyozidi kung’ara alihama Sinza Madukani na kuhamia Sinza Mori
jirani na baa ya Meeda upande wa kulia kama unatoka kituo cha Mori kuelekea Mlimani City. Nyumba hizi mbili hakuwa amepanga nyumba nzima, bali alikuwa akiishi upande na failia yake huku wakishea geti na wapangaji wengine.
Mwaka jana ndipo alipohamia katika nyumba nyingine iliyopo Sinza Mori jirani na Hotel ya Wanyama ambapo anaishi mpaka
sasa. Swali linakuja kwamba kwa mtu anayemiliki bilioni moja au nusu
bilioni anawezaje kuishi nyumba kamili isiyokuwa yake?
Nyumba nyingine inayodaiwa
Kumilikiwa na Diamond ni aliyonunua Mwananyamala ambapo kwa mujibu wa watu wanaoifahamu wameeleza kuwa inahitaji marekebisho makubwa
ili iweze kuitwa nyumba ya mtu mwenye utajiri wa bilionimoja. Taarifa
kutoka mitaa yote ya Mwananyamala na Kinondoni, hakuna mtaa ulionunuliwa
na Diamond.
Kuazima magari
Hivi karibuni Diamondamewahi kukiri kupewa gari na mfanyabiashara maarufu Mohamedi Kiumbe ‘Chief Kiumbe’.
Uchunguzi wa swahilitz umebaini kuwa gari hilo hakupewa kama alivyoeleza
bali aliazima kwa gia ya kutaka kulinunua, baadhi ya rafiki zake
wanasema kwamba alitaka kutumia matangazo ya vyombo vya habari kuhusu
kupewa gari hilo ili iwe rahisi Chief Kiumbe kuingia mkenge ameoewa gari hilo na kaka yake Chief Kiumbe. Gari hilo linalokadiriwa kuwa na thamani ya shilingi milioni 200 kitu ambacho hata chizi hawezi kukitoa bure.
CREDIT :dj joker
0 comments:
Chapisha Maoni