Watu
wawili wanaosadikiwa kuwa ni wezi wameuwawa leo na wananchi wanaotajwa
kuwa na hasira kali katika mtaa wa Mayila kata ya Nyihogo wilayani
Kahama Mkoani Shinyanga.Tukio hilo la mauaji limetokea leo majira ya saa tisa alasiri baada ya vijana hao kuhisiwa kuhusika na matukio ya wizi ambayo yamekuwa yakitokea katika eneo hilo mara kwa mara na kuwakosesha amani wananchi.
Gari la polisi wilaya ya Kahama likiwa limezungukwa na wananchi eneo la Tukio
Kwa mujibu wa Diwani wa Kata ya Nyihogo Amos Sipemba, aliyefika eneo la tukio mara baada ya mauwaji hayo, amesema hadi sasa mmoja wa marehemu ametambulika kwa jina la Joseph Bakuku huku mwingine akiwa bado hajafahamika.
Sipemba amesema huenda kufanyika kwa mauwaji hayo kunatokana na wananchi hao kuwahisi vijana hao kuhusika katika matukio mawili ya uvamizi yaliyotokea usiku wa kuamkia jana katika kata hiyo na kuripotiwa ofisini kwake.
Jeshi la Polisi wilayani Kahama limethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba miili ya marehemu hao imehifadhiwa katia chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya Wilaya ya Kahama, huku uchunguzi wa tukio hilo ukiendelea.
0 comments:
Chapisha Maoni