Yeleuuuwi! Siku chache baada ya msanii wa sinema na muziki Bongo, Zuwena
Mohamed ‘Shilole’ kujinadi na mchumba wa Kizungu aliyejulikana kwa jina
moja la Ankar, siri imefichuka kwamba jamaa huyo ni mwanaume tata.
Kikizungumza na Ijumaa Wikienda kutoka London, Uingereza, wikiendi
iliyopita, chanzo hicho makini kilisema mwanaume ambaye hivi karibuni
Shilole alijinadi kuwa ni bwana’ke siyo kwani huko London baadhi ya watu
wanamfahamu kama mwanaume tata kijinsia.
“Yule jamaa anapenda sana kukaa na wanawake, sijawahi kumuona na wanaume
wenzake, kazi kukata tu mauno na wanawake. Nilishangaa sana Shilole
kusema eti ni mchumba’ke wakati hapa London (Uingereza) ni maarufu sana
kwa kushiriki pati za wanawake.
“Maskini Shilole, pale imekula kwake, hakuna chochote,” kilisema chanzo hicho.
Baada ya kunyetishiwa habari hizo, gazeti hili lilimtafuta Shilole ambapo alikuwa na haya ya kusema:
“Jamani imeniuma sana kwani nilikuwa sijui, nimeligundua hilo baada ya
kuambiwa na watu, nilipigiwa simu kutoka Uingereza kwamba yule mwanaume
siyo hivyo sina mpango naye tena kwa kweli,” alisema Shilole anayetamba
na kideo cha Nakomaa na Jiji.





0 comments:
Chapisha Maoni