Ni nadra sana kwa Mastaa wengi wa
Tanzania kukubali kusema kiwango anachopata kwa mwezi kutokana na kazi
yake ya umaarufu ila kwa Mzee Majuto ni kinyume, amekubali kusema kila
kitu kwenye kipato cha movie zake za vichekesho ambazo mpaka sasa ndio
zinashika namba 1 kwa mauzo Tanzania?
Kwa sababu ni kiapo cha
millardayo.com kuhakikisha chochote ambacho ni stori unakipata, imempata
Mzee huyu Mbembe kutoka Kigoma akiwa ni mzaliwa wa Tanga umri ukiwa
miaka 65 na kukubali kuzungumza kwenye hii Exclusive interview.
Akiwa ni baba wa watoto tisa,
anakwambia ‘kwenye movie za kuigiza sasa hivi kama mtu akitaka
kunishirikisha ni lazima unilipe milioni nane kutoka milioni 2 au tatu
nilizokua nazikusanya mwanzoni, hii bei nimeibadili kuanzia mwezi
September 2013, mimi kadri ninavyocheza movie nyingie za kushirikishwa
ndio nazidi kujipunguzia kipato changu kwa mwezi kutoka kampuni ya STEPS
iliyoniajiri’
‘Mpaka sasa nimecheza movie zaidi ya
600 toka nimeanza kuigiza za kushirikishwa na zangu mwenyewe, nilianza
kulipwa zaidi ya milioni moja kwenye movie toka mwaka 2007/2008 baada ya
kuwa na kampuni ya Ally Riyami ambae alikua ananilipa shilingi laki
sita kwa kila movie ya Comedy kwa hiyo kwa mwezi napata mpaka kwenye
milioni 6 au saba kutokana na idadi ya movie nitakazoigiza’ – Mzee
Majuto
‘kwa sasa hapa Steps nalipwa kuanzia
milioni 17 mpaka 20 kwa mwezi, ni malipo mazuri sana ambayo napata kila
mwezi na nimepangiwa kucheza movie 9 kwa mwaka lakini kule Ally Riyami
kwa mwezi ndio nilikua nacheza hizo movie 10, yani unacheza movie mpaka
unasikia kizunguzungu…. kwa sababu nilitakiwa kucheza movie 1 kila baada
ya siku tatu ila kwa sasa kwenye mkataba wa Steps nacheza movie moja ya
kampuni na moja ya nje ya kampuni, maisha mazuri’ – Mzee Majuto
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)

0 comments:
Chapisha Maoni