
Gazeti la chama tawala cha china, People’s Daily ambalo
limezoea kuwa kitovu cha kusambasa habari, sasa limejikuta likiwa
habari baada ya watu wenye fikra za kitukutu kuona jengo jipya la gazeti
hilo limefanana na nyeti za kiume.
Jengo hilo lenye urefu wa mita 150, hivi
sasa bado linaendelea kujengwa jijini Beijing. Kutokana na muundo huo
usiokua wa kawaida, picha za kibunifu zikaanza kuibuka katika website
ambayo ni kama “Twitter ya China,” inayoitwa Sina Weibo.

Watu wengi wameeleza kuwa kwa kutumia
ubunifu kidogo tu wa photoshopping, unaweza kuambatanisha picha ya jengo
hilo, ambalo raia wamelipa nickname“Giant Pen*s” au “Uume mkubwa,” katikati ya “miguu” ya
jengo lingine maarufu nchini humo ambalo ni makao makuu ya kituo cha TV
cha China Central Television (CCTV,) linalojulikana kwa nickname ya “Big Und*rpants” building au Jengo la Chupi Kubwa.

Habari za utani huo zilifikia wakubwa
nchini humo ambao walikerwa na kuamua kuwaharibia watu raha zao kwa
kuamuru website ya Sino Weibo ku-block search zote zinazotafuta picha au
habari za jengo hilo.
Kwa sasa Wachina wakitafuta jengo hilo, wanakutana na ujumbe “kuendana na sheria, kanuni na sera husika, matokeo ya utafutaji wako (search results) hayawezi kuonyeshwa."
Mwandishi wa Reuters, Anita Li amesema “hii
inaonyesha frustrations miongoni mwa vijana watumiaji wa internet
nchini China, na pia inaonyesha ni kiasi gani “wakubwa” wako sensitive
kwa hata vitu vidogo vya kipuuzi online.”
0 comments:
Chapisha Maoni