MSANII
wa muziki wa kizazi kipya anayeunda kundi la Makomandoo Fredy Wayne
ambaye alikuwa akitoka kimapenzi na Jacqueline Wolper amesema ameachana
naye na sasa yupo na nyota mwingine wa filamu, Kajala Masanja.
Akizungumza FC hivi karibuni, Fredy alisema msanii huyo amemchanganya
mno kimapenzi kiasi kwamba ameamua kumwandikia wimbo unaitwa Ushaniroga,
kuonyesha ni jinsi gani amedata naye.
“Siyo
siri jamani ndiyo kashaniroga, nampenda na yeye kaonyesha upendo wake
kwangu, nipo naye na kuhusu huyo Jack Wolper ni maisha tu, ni rafiki
zangu, huwa naona nao katika maeneo tunapiga kiss, ni vitu vya kawaida
lakini sasa niko na Kajala,” alisema.
Hata hivyo, wadada hao wawili wanaofanya vizuri katika tasnia ya filamu Bongo hawakuweza kupatikana ili kuzungumzia habari hiyo ambayo ni gumzo ya jiji kwa sasa.

Kajala Masanja aliyempora Jack Bwana

Jack Wolper

Fredy Wayne mwanamuziki aliyewachanganya Jack na Kajala

Kajala Masanja
Hata hivyo, wadada hao wawili wanaofanya vizuri katika tasnia ya filamu Bongo hawakuweza kupatikana ili kuzungumzia habari hiyo ambayo ni gumzo ya jiji kwa sasa.

0 comments:
Chapisha Maoni