Mpenzi
msomaji wa safu hii, juma lililopita tuliona na kujifunza baadhi ya
dalili za mpenzi asiye na penzi la dhatiu kwako, hii tunajikita kujua
walau faida tisa za kufanya ngono.
Ngono au tendo la ndoa lina faida kubwa katika mwili wa binadamu ambazo
ni zaidi ya kustarehesha ama kustareheshwa hasa linapofanywa na watu
wazima na tendo hilo ukizidisha unaweza kupata madhara kiafya .
1. Mzunguko wa Damu.
Tendo la ndoa huongeza kasi ya mzunguko wa damu mwilini kutokana na
kuongezeka kwa mapigo ya moyo ambayo huboresha mzunguko huo wa damu pale
unapopumua wakati wa kufanya tendo hilo.
2. Mazoezi ya mwili.
Watu wengi hawafanyi mazoezi lakini kufanya ngono ni moja ya mazoezi ya
mwili ambapo unatakiwa kwa wiki moja asizidishe kufanya ngono mara tatu
jambo ambalo litakusaidia kupunguza kiasi cha mafuta mwilini pia
ukifanya hivyo kwa kipindi cha mwaka mmoja ni sawa na kukimbia maili 75
na tendo hilo huongeza karibia vizalisha nguvu 150 kwa nusu saa ambayo
ni sawa na kukimbia dakika 15 uwanjani.
3. Maumivu
Unapofanya mapenzi homoni iitwayo oxytosin huzalishwa mwilini ambayo
hupelekea kuzalishwa kwa homoni iitwayo endorphin ambazo huwezesha
kupunguza maumivu mwilini ikiwemo uvimbe, maumivu ya shingo na kichwa
ambapo ukiona vitu hivyo vinakusumbua fanya mapenzi.
4. Mafuta yenye kileo
Huweka uwiano wa mafuta yenye kileo (Cholesterol) nzuri na mbaya na hupunguza kwa uwiano sawa kiasi cha mafuta mwilini.
5. Huondoa Maji yenye madhara
Tendo la ndoa la mpangilio huondoa uzalishaji wa majimaji yanayozalishwa kwenye prostate ambayo huwa na madhara kwa binadamu.
6. Usingizi mnono
Hakuna ubishi kwa yeyote aliyewahi kufanya ngono kuwa aliwahi kupata
usingizi mnono isivyo kawaida hasa baada ya shughuli ambayo hata mnyama
Simba angeingia mahala hapo pa faragha hakuna hata mmoja ambaye angeweza
kuacha tendo hilo na kumkimbia Simba.
Kufanya mapenzi na kuupumzisha mwili kabla ya kuanza tena tendo hilo
hasa kwa wanaume ni jambo muhimu ambapo utaupa mwili auheni ya kutuliza
akili na kurekebisha mzunguko wa damu mwilini ambapo baadaye ukitaka
kulala utalala swadakta…….
7. Kudumisha ujana
Homoni iitwayo DHEA huzalishwa mwilini ambayo husaidia msisimko
kuongezeka ambapo mwanadamu anayefanya mapenzi huongezewa ufahamu,
kuimarisha mifupa, mishipa ya moyo na hata kuzuia wapinzani wa kazi za
mishipa ya fahamu na hupunguza baridi na mafua na watu wanaofanya
mapenzi huelezwa kuwa mara kadhaa huonekana vijana hata kama umri
utakuwa umekimbia.
8. Homoni za kiume na za kike kuongezeka
Uzalishaji wa homoni za kike na kume huongezeka mara dufu ambapo kwa
mwanaume humsaidia kuimarika kwa homoni ya kiume ambayo husaidia
kuimarisha mifupa na miduli na kwa mwanamke tendo al ndoa humwongezea
honi ambayo inatunza tissue za sehemu ya uke na humsaidia kupokea
mapenzi na kuwajibika awapo mahala husika na mwenzi wake.
Mpenzi msomaji wangu bila shaka umeanza kupagawa baada ya kuona walau
faida chache za kufanya mapenzi, sasa wiki lijalo tutaangalia dalili za
mwanamke anapotaka ngono.
CREDITS: DJ JOKER MZA TZ.
0 comments:
Chapisha Maoni