Pages

TUNAJIUSISHA NA HABARI ZA AINA ZOTE NDANI NA NJE YA BONGO VILEVILE TUNAKODISHA VYOMBO VYA MUZIKI NA P.A MAENEO YOTE YA JIJI LA MWANZA NA NJE YA JIJI LA MWANZA KARIBUNI SANA

ROSE NDAUKA AJIFUNGUA MTOTO WA KIKE SOMA ZAIDI..

Rose ndauka ajifungua mtoto wa kike.
MSANII wa filamu, Rose Ndauka amejifungua mtoto wa kike Jumapili iliyopita katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam na kusisitiza, amefanana na baba yake.
Ndauka ambaye miezi michache iliyopita, alitangaza kusimama kuigiza kwa muda wa mwaka mmoja ili ajitathmini alijifungua mtoto huyo kwa operesheni.
Katika mazungumzo na Mwanaspoti, Ndauka alisema: “Namshukuru Mungu, nimefanikiwa kujifungua salama, mtoto mwanamke.”
“Ni faraja kwangu kwa sababu nimepata mwenzangu na amefanana na baba yake mzazi (Pichani),” alisema Ndauka bila kutaja jina la baba wa mtoto huyo.
Ndauka ni mwigizaji maarufu wa filamu anayekubalika katika tasnia hiyo huku akitamba na kazi zake mbalimbali zikiwamo, Bad Girl, Fall in Love na nyinginezo.

0 comments:

Chapisha Maoni