![]() |
| Picha ya Wayne Rooney ikionyesha jinsi alivyoumia kichwani |
Straika
wa Uingereza, Wayne Rooney amepost picha mtandaoni picha inayoonyesha
jinsi alivyojeruhiwa kichwani, majeraha yaliyomfanya akose mechi za
kuwania kufuzu kombe la Dunia.
Nyota
huyo mwenye umri wa miaka 27, alikosa mechi ya Manchester United wakati
ilipocheza dhidi ya Liverpool (Waliyokula kichapo cha 1-0) Jumapili
iliyopita baada ya David Moyes kuthibitisha kuwa amepata majeraha
kichwani kufuatia kugongana kwa bahati mbaya na mchezaji mwenzake Phil
Jones walipokuwa kwenye mazoezi.
Moyes
alieleza kuwa ana imani Rooney atapona mapema na kujiunga na wenzake
kwenye timu ya Taifa itakayocheza dhidi ya Moldova na Ukraine.
Rooney
ameweka picha inayoonyesha majeraha yake kwenye ukurasa wake wa
facebook Jumatano jioni ikifuatiwa na maelezo machache kama
yanavyoonekana kwenye ayah ii hapa chini.
"Baadhi
ya watu wanajiuliza kama nitaitumikia Uingereza kipindi hiki ama la, ki
ukweli nimeamua kujito kwenye michezo miwili ya kuwania kufuzu kombe la
Dunia," aliandika.
![]() |
| Ukurasa wa Facebook wa Wayne Rooney ukionyesha jinsi alivyoandika kuhusu majeraha yake ya kichwani |
"Hakuna
shaka, napenda kuwa pamoja na wenzangu kuwania kufuzu kucheza kombe la
Dunia. Nina imani watu wakiona picha hii wataelewa ni kwanini siwezi
kucheza kipindi hiki."
Mchezaji mwenzake Theo Walcott alieleza jana kuhusu kidonda hicho "kinafanana na majeraha ya kwenye filamu za kutisha".
Uingereza
itaumana na Moldova na Ukraine, kwa sasa iko nyuma ya vinara Montenegro
kwa point 2 lakini ikiwa na mchezo mmoja mkononi.
Rooney,
ambaye alihusishwa sana na uhamisho kwenda Chelsea kabla dirisha la
usajili halijafungwa, aliamua kubaki Manchester United.
Lakini
majeraha hayo yanamaanisha Rooney, aliyeichezea England mara 84 na
kufunga magoli 36, atakosa mechi kadhaa za kuwania kufuzu kombe la dunia
wakati wachezaji wenzake Danny Welbeck, na nyota wa Liverpool Daniel
Sturridge watakaposhuka dimbani.


0 comments:
Chapisha Maoni