Mmoja wa waigizaji mahiri wa filamu hapa nchini Elizabeth Michael
akijulikana zaidi kwa la kisanii kama Lulu akiwasili kwenye semina ya
kamata fursa Twendzetu,ndani ya ukumbi Gold Crest,jijini Mwanza asubuhi
hii,ambapo pia atazungumzia mambo kadhaa mbalimbali kwenye semina
hiyo,ambayo itawakutanisha Naibu Waziri wa Mawasiliano,Sayansi na
Teknolojia,Mh Januari Makamba,Mbunge wa jimbo la Kigoma Kaskazini na
watoa mada wengine mbalimbali. 

Naibu Waziri wa Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia,Mh Januari Makamba
akiwa ameambatana na Naibu Waziri wa Nishati na Madini,Mh Stephen Masele
(mwenye miwani) akisalimiana na Mkurugenzi wa Benki ya Wanawake
Tanzania (TWB),Bi.Magreth Chacha walipokuwa wakiwasili kwenye semina ya
kamata fursa Twendzetu,ndani ya ukumbi Gold Crest,jijini Mwanza asubuhi
hii,pichani kati ni Mkurugenzi wa vipindi na uzalishaji Clouds Media
Group,Bwa.Ruge Mutahaba.
Baadhi ya Wakazi wa mji wa Mwanza na vitongoji vyake wakiwa
wamejitokeza kwa wingi kwenye semina ya kamata fursa Twendzetu,ndani ya
ukumbi Gold Crest,jijini Mwanza asubuhi hii.




0 comments:
Chapisha Maoni