Majambazi saba akiwemo mmoja ambaye amevalia sare za polisi wameiteka
benki ya I&M jijini Dar es Salaam na kuchukuwa fedha zinazohisiwa
kuwa ni zaidi ya shilingi milioni 150 na kutokemea kusikojulikana.
Tukio hilo limetokea katika benki hiyo iliyoopo katika makutano ya mtaa
wa Indira Gandi na Mosque ambapo baadhi ya mashuhuda wameelezea tukio
hilo lilivyokuwa.
Akizungumza katika eneo la tukio kamanda wa polisi mkoa wa Ilala kamanda
Marieta Minagi amesema bado wanaendelea kufanya uchunguzi wa tukio
lenyewe ingawa mpaka sasa ni kama milioni zaidi 150 zinahisiwa
kuibiwa.
Naye mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Said Meki Sadiki akiwa katika eneo
hilo amesema matukio ya Kuiba fedha katika benki yanazidi kushamiri na
hivyo kuna haja ya taasisi husika kujipanga upya.
Hata hivyo ITV ilishuhudia baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo
wakipandishwa katika gari la polisi lenye namba za usajili T220 AMV na
kuondoka nao kwa ajili ya mahojiano zaidi

0 comments:
Chapisha Maoni