Msanii Tundaman amejikuta akiambulia
aibu ya mwaka baada ya kujitosa nusu uchi mtaani akiwakwepa askari
polisi ambao walivamia kwake leo asubuhi kwa lengo la kumkamata....
Chanzo cha Tunda man kusakwa na
polisi ni deni la sh. laki nane ambazo alikopa mwanzoni mwa mwaka huu
kwa mwanadada mmoja ( jina kapuni)....
Taarifa zinadai kwamba, baada ya
kupewa hela hiyo, Tunda man aligeuka kisima cha matusi ya nguoni kwa
mrembo huyo. Kila akipigiwa simu alikuwa hapokei, na akipokea ni matusi
ya nguoni.....
Baada ya hali hiyo, mwana dada huyo
aliamua kulifikisha swala lake polisi ambapo Tundaman alikamatwa. Akiwa
mikononi mwa polisi, msanii huyo aliomba apewe nafasi ya kulilipa deni
lake kwa awamu tatu kuanzia tarehe 12/8/2013
Baada tarehe hiyo, Tundaman hakuweza
kulipa kiasi chochote na wala hakutoa ushirikiano wowote, hali
iliyomfanya mwanadada huyo arudi kuripoti polisi....
Polisi walianza jitihada za kumsaka
ambapo leo majira ya saa nne asubuhi walivamia kwake ( Tabata Savana )
kwa lengo la kumkamata.....
Bahati nzuri au mbaya, Tundaman
alifanikiwa kuwatoroka polisi akiwa na bukta tu ( kwa mujibu wa
mashuhuda) na kutokomea kusikojulikana...
Ifuatayo ni HATI YA MAKUBALIANO yao ambayo mpekuzi wetu amefanikiwa kuipata....


0 comments:
Chapisha Maoni